Friday 9 November 2018

LIFAHAMU CHIMBUKO LA NENO UYOGA (EKITUZI)

Ukiangalia majina ya uyoga mengi kama si yote yanatokana na umbile au mwonekano:
1: EKINYAMUJEGEJE (huwa ni 'laini sana,' jegulijeguli')

2: ENYAMUKUNDI (kwa sababu ya kipele ni kikubwa juu kabisa. 'omukundi' katikati.Q

3: EMPEEFU yaani 'iliyopauka' kutokana na mwonekano wa 'kijivu yenye kupauka'.

Nafikiri pia Ukisema 'Ekituzi'= Ekilikutura/ekilikututura=kitu kinachoenda au kutokea = nafikiri ilitokana na namna uyoga unavyoota,yaani nkitutura kuluga omwiitaka.. Kwahiyo 'Nkitutura'= ekilikututura =Ekituzi.

TUKUTANE DECEMBER 25!
#mulebamiamia
Kizalendo Zaidi.

Thursday 8 November 2018

EMPEFU

Hii ni aina nyingine ya uyoga wa asili unaopatikana wilayani kwetu Muleba, Ukiwa maeneo ya Muleba mjini Eneo liloongoza kwa upatikanaji wake  ni KASHAKO na huu ndo msimu wake Hivyo wale mnaotembelea mashambani usikipite kichuguu bila kutupia jicho.

Kwa wale msio ifahamu KASHOKO
Hii ipo KATA YETU YA MULEBA BUKONO Maarufu kama KASHAKO AU KISHENYI pana historia yake. Zamani walichimba udongo maeneo hayo alafu wanausiliba ukutani kama lip wengine wakitumia nyasi ambazo zimeshakariwa ndani ya nyumba na kutupwa shambani mabaki yake (Esingo) udongo huu una kuwa na rangi ya Majivu ukisha kauka wakati mwingine unaweza dhania imechanganywa na cement kwa uzuri wake but ni zamani KIDOGO na asiri inapotea.

TUKUTANE DECEMBER 25
#mulebamiamia
Kizalendo Zaidi.

Tuesday 6 November 2018

EGABELI " BAISKELI YA MITI"

EGABELI!

Miongoni mwa michezo inayo chezwa na watoto wa vijijini kwetu ni kuendesha baiskeli ya miti maarufu kama "EGABELI"
Utamu wa kuendesha hii biskeli ya miti hunoga zaidi pale unapofika kwenye mteremko maana unaseleleka tu kwa raha zako!

TUKUTANE DECEMBER 25
#mulebamiamia
Kizalendo Zaidi.

Monday 5 November 2018

EKITUZI (UYOGA)

Huku kwetu Uyoga unaitwa EKITUZI na umepewa majina ya kiasili kulingana na umbo lake kwa mfano kuna aina ya "ENYAMKUNDI" "EMPEFU" n.k

Uyoga wa kwetu ujiotesha wenyewe maporini kwa msimu flani sio wakati wote nakama ilivyo ada kile kitendo cha kwenda porini kutafuta uyoga wakati wa msimu wake hiutwa "OKWENJA"

Kitaalamu hizi hapa ni faida za uyoga:

1: Uyoga unalishe kama protini inayolingana na ile ipatikanayo kwenye maziwa, samaki na kunde. Pia utapata vitamini B, C, na D, na madini ya joto, phosphoras, chuma na potashi.

2: Uyoga husadikika kutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, moyo, shinikizo la damu na figo.

Tukutane December 25
#mulebamiamia
Kizalendo Zaidi

Saturday 3 November 2018

MULEBA ZAIDI YA UIJUAVYO!

Kwa taarifa yako tu Eneo linalo ongoza kupigiwa picha na watu wengi zaidi kuliko sehemu nyingine yeyote wilayani Muleba liko maeneo ya Kagoma. Kama inavyo onekana kwenye picha.

Watu wanaopigia picha eneo hili ni Wageni wanaoingia na kutoka wilayani Muleba, lakini pia zaidi ya asilimia 90 ya ndoa zinazofungwa wilayani Muleba Maharusi wake wamekua wakilitumia kupigia picha za ukumbusho.

Wale wazee wa fursa mnasubili nini kuboresha hili eneo?

Friday 23 February 2018

ZIMEBAKI SIKU 8 TU.

Mambo ni Moto wakazi wa muleba kuja kushuhudia ligi kubwa ya mpira wa miguu wilayani humo ambayo itashirikisha timu 16 na 15 ni kutoka wilayani Muleba na 1 kutoka kyaka.

Saturday 7 October 2017

MSIMU WA SOKA MULEBA

IMEDHIBITISHWA!

MULEBA STARS kukipiga na NDANDA FC tarehe 30/10/2017.
Wakazi wa Muleba na vitongoji vyake wakae mkao wa kula kuja kuzishuhudia timu zinazo cheza ligi kuu ya Tanzania bara kwenye uwanja wa Zimbihile.

Mtanange wa kwanza utapigwa tarehe 30/10/2017 Mwambie na mwenzio msimu wa soka umrudi tena kwa staili mpyaaa!

MSIMU WA SOKA 30/10/2017
MULEBA MiaMia!
Kizalendo Zaidi.

MADEREVA WA CANTER MULEBA!

Kama ulikua haujui Kwa Muleba mjini Madereva wengi wanao endesha magari aina ya Canter wanatokea kijiji kimoja kinaitwa Malahala.

Msimu wa soka unakuja 30/10/2017
MULEBA MiaMia!
Kizalendo Zaidi.

Friday 6 October 2017

WAFAHAMU WATU WALIO WAHI KUWA WENYEVITI WA CCM WILAYA MULEBA.

Jana wanachama wwa CCM wilaya ya Muleba walimchagua bwana Athumani Kahara kuwa Mwenyekiti Mpya wa chama hicho duru zinasema upinzani ulikua mkubwa mno ila demokrsia imetawala.

Kwa wanao mfahamu bwana Athumani kwa Uchapakazi na Uhodari wa kufanya kazi za jamii basi wanaungana na mimi kuwa ccm wamesajiri kifaa. wale walio kua shuke ya msingi Rubungo miaka ya 1990's watakubaliana na mimi yale machachari yake wakati anagombea kuwa kaka mkuu lakini pia alivyo kuwa akiwaongoza wanafunzi wenzake baada ya kushinda.

Hawa ni viongoi walio mtangulia Bwana Athumani Kahara kwenye nafasi hiyo 

1.Ernest Masilingi
2.Peter Kyabona
3.Simon Katarama
4.Muhaji Bushako.
Tukumbuke nini toka kwao? Muleba ni yetu sote!

MULEBA MiaMia!
Kizalendo Zaidi.

Thursday 5 October 2017

FURSA ZILIZOPO MKOA WA KAGERA KATIKA SEKTA YA UVUVI.

Mkoa wa Kagera una eneo la maji lenye ukubwa wa kilomita za mraba 10,655 sawa na asilimia 27, jiografia nzuri, maeneo chepechepe yenye udongo unaotunza maji na vyanzo vingi vya maji (water bodies) kama vile mto Kagera, Mto ngono, mto Ruvuvu, mto Kanoni, Ziwa Victoria na maziwa mengine madogo madogo 15. Mkoa huu wa Kagera unasifika na kuwa Mkoa wa kwanza nchini Tanzania na wa pekee wenye maziwa madogo madogo (Satellite Lake) mengi yanayofikia 15 kama yafuatayo.

Ziwa Burigi Ziwa Burigi linapakana na Wilaya tatu ambazo ni Muleba, Karagwe na Biharamulo Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina samaki wengi aina ya Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haprochromis), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Rwakajunju Ziwa Rwakajunju linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 27.72. Baadhi ya samaki waliomo ni pamoja na Furu (Haprochromis), Sato (Oreochromis esculentus na Variabilis), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Kamakala Ziwa kamakala linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haprochromis), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Ikimba Ziwa Ikimba linalinapatikana Wilaya ya Bukoba Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 38.09. Baadhi ya samaki waliomo ni pamoja na Furu (Haplochromines), Sato (Oreochromis esculentus), Kamongo (Protopterus catastoma) na Kambale (Clarius gariepinus). Ziwa hili linapatikana Bukoba Vijijini Mkoa wa Kagera. Baadhi ya changamoto zilizopo Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Rushwa Ziwa Rushwa linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 10.08. Baadhi ya samaki waliomo ni pamoja na Sato (Oreochromis esculentus, leocosticus, niloticus, variabilis na Tilapia zilii), Kamongo (Protopterus aethhiopicus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Melula Ziwa Melule liko Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 15.21. Samaki waliomo ni pamoja na Sato (Oreochromis esculentus na niloticus), Furu (Haplochromines) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Katwe  Ziwa katwe linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina ukubwa wa km2 2.23. Ziwa hili lina aina 6 za samaki ambao ni pamoja na Sato (Oreochromis leocostictus), Furu (Haprochromines), Kamongo (Protopterus aethiopicus), Kambale (Clarius gariepinus), (Momyrus) na Gogogo (S.afrofischeri). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Luko Ziwa Luko linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa hili lina samaki wengi aina nyingi ya Sato (Oreochromis esculentus), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Kalenge Ziwa Karenge linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Ziwa lina aina 9 za samaki ambao ni Sato (O.leocostictus, niloticus na variabilis), Furu (Haplochromines), B.profundus na B.sadleri, Kambale (Clarius gariepinus na C.alluaudi) na Gogogo (S.afrofischeri). Ziwa hili linakumbwa na changamoto ya Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumu na magugu maji.

 Ziwa Mitoma Ziwa Mitoma linapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Kuna aina 5 za samaki ambao ni (B.sadleri), Kambale (Clarius gariepinus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus aethiopicus) na Gogogo (Synodontis afrofischeri).

Ziwa Kaburi Ziwa Kaburi linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Kamongo (Protopterus aethiopicus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zilinazopo ni Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na kilimo na magugu maji.

Ziwa Kitete, Ziwa Kitete linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Ziwa hili Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Kabindi Ziwa Kabindi linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Ziwa hili Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Ngoma Ziwa Ngoma linapatikana Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki wengi aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus). Baadhi ya changamoto zinazolikumba Ziwa hili ni pamoja na Uvuvi usioendelevu, uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi na magugu maji.

Ziwa Rumanyika Ziwa Rumanyika linapatikana katika hifadhi ya rumanyika Wilaya ya Kyerwa. Ziwa hili linasifika kwa kuwa na samaki aina Sato (Oreochromis esculentus), Furu (Haplochromines), Kamongo (Protopterus) na Kambale (Clarius gariepinus).

MSHINDI NI ATHUMANI KAHARA.

Mtokeo yametoka Mwenyekiti mpya wa ccm wilaya ya Muleba ni Mr Athumani Kahara.

wenyewe wanasema OMUHIGO GWA INDUKA AKAMI KABINGA EMBWA.

MULEBA MiaMia!
Kizalendo Zaidi.

WAGOMBEA WA NAFASI YA UENYEKITI CCM WILAYA YA MULEBA.

Pichani Kushoto ni Athumani Kaala na Cosmas Timanywa moja wapo kati ya hawa anatakiwa aibuke mshindi kwenye kura zinazo endelea kupigwa kwenye ukumbi wa Waisuka ulioko Muleba mjini.

Huko joto limepamba moto kutoka kwenye kambi zote mbili taarifa ya uchunguzi juu ya mchakato mzima itakuja baada ya matokeo kutoka.

Tutaendelea kukujuza kinacho endelea.

MULEBA MiaMia!
Kizalendo zaidi.

MH MWIJAGE AHUDHURIA MKUTANO WA CCM WILAYA MULEBA.

Mh Waziri Mwijage ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Muleba Kaskazini kupitia tiketi ya ccm naye yupo kwenye mkutano unaoendelea kwenye ukumbi wa Waisuka Wilayani Muleba.

MULEBA MiaMia!
Kizalendo Zaidi.

UCHAGUZI WA MWENYIKITI CCM WILAYA MAMBO NI MOTO.