Friday 9 November 2018

LIFAHAMU CHIMBUKO LA NENO UYOGA (EKITUZI)

Ukiangalia majina ya uyoga mengi kama si yote yanatokana na umbile au mwonekano:
1: EKINYAMUJEGEJE (huwa ni 'laini sana,' jegulijeguli')

2: ENYAMUKUNDI (kwa sababu ya kipele ni kikubwa juu kabisa. 'omukundi' katikati.Q

3: EMPEEFU yaani 'iliyopauka' kutokana na mwonekano wa 'kijivu yenye kupauka'.

Nafikiri pia Ukisema 'Ekituzi'= Ekilikutura/ekilikututura=kitu kinachoenda au kutokea = nafikiri ilitokana na namna uyoga unavyoota,yaani nkitutura kuluga omwiitaka.. Kwahiyo 'Nkitutura'= ekilikututura =Ekituzi.

TUKUTANE DECEMBER 25!
#mulebamiamia
Kizalendo Zaidi.

Thursday 8 November 2018

EMPEFU

Hii ni aina nyingine ya uyoga wa asili unaopatikana wilayani kwetu Muleba, Ukiwa maeneo ya Muleba mjini Eneo liloongoza kwa upatikanaji wake  ni KASHAKO na huu ndo msimu wake Hivyo wale mnaotembelea mashambani usikipite kichuguu bila kutupia jicho.

Kwa wale msio ifahamu KASHOKO
Hii ipo KATA YETU YA MULEBA BUKONO Maarufu kama KASHAKO AU KISHENYI pana historia yake. Zamani walichimba udongo maeneo hayo alafu wanausiliba ukutani kama lip wengine wakitumia nyasi ambazo zimeshakariwa ndani ya nyumba na kutupwa shambani mabaki yake (Esingo) udongo huu una kuwa na rangi ya Majivu ukisha kauka wakati mwingine unaweza dhania imechanganywa na cement kwa uzuri wake but ni zamani KIDOGO na asiri inapotea.

TUKUTANE DECEMBER 25
#mulebamiamia
Kizalendo Zaidi.

Tuesday 6 November 2018

EGABELI " BAISKELI YA MITI"

EGABELI!

Miongoni mwa michezo inayo chezwa na watoto wa vijijini kwetu ni kuendesha baiskeli ya miti maarufu kama "EGABELI"
Utamu wa kuendesha hii biskeli ya miti hunoga zaidi pale unapofika kwenye mteremko maana unaseleleka tu kwa raha zako!

TUKUTANE DECEMBER 25
#mulebamiamia
Kizalendo Zaidi.

Monday 5 November 2018

EKITUZI (UYOGA)

Huku kwetu Uyoga unaitwa EKITUZI na umepewa majina ya kiasili kulingana na umbo lake kwa mfano kuna aina ya "ENYAMKUNDI" "EMPEFU" n.k

Uyoga wa kwetu ujiotesha wenyewe maporini kwa msimu flani sio wakati wote nakama ilivyo ada kile kitendo cha kwenda porini kutafuta uyoga wakati wa msimu wake hiutwa "OKWENJA"

Kitaalamu hizi hapa ni faida za uyoga:

1: Uyoga unalishe kama protini inayolingana na ile ipatikanayo kwenye maziwa, samaki na kunde. Pia utapata vitamini B, C, na D, na madini ya joto, phosphoras, chuma na potashi.

2: Uyoga husadikika kutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, moyo, shinikizo la damu na figo.

Tukutane December 25
#mulebamiamia
Kizalendo Zaidi

Saturday 3 November 2018

MULEBA ZAIDI YA UIJUAVYO!

Kwa taarifa yako tu Eneo linalo ongoza kupigiwa picha na watu wengi zaidi kuliko sehemu nyingine yeyote wilayani Muleba liko maeneo ya Kagoma. Kama inavyo onekana kwenye picha.

Watu wanaopigia picha eneo hili ni Wageni wanaoingia na kutoka wilayani Muleba, lakini pia zaidi ya asilimia 90 ya ndoa zinazofungwa wilayani Muleba Maharusi wake wamekua wakilitumia kupigia picha za ukumbusho.

Wale wazee wa fursa mnasubili nini kuboresha hili eneo?